‘ujenzinamakazitanzania’ ni blog inahusisha shughuli zote za ujenzi na makazi hapa
Tanzania. Ni blog inayohusisha wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi kama vile Wizara ya ardhi
,Nyumba na Makazi;wakandarasi(Contractors) wachora ramani na wabunifu (Architects),wakadiriaji
gharama za ujenzi (Quantity surveyors),washauri(Consultants),wahandisi(Engineers),wasambazaji
na wauzaji bidhaa za ujenzi,mafundi mbalimbali na pia wamiliki wa nyumba,majengo
au ardhi.
Katika blog
hii,utaweza kujionea picha na matukio
mbalimbali ya ujenzi na makazi; na pia utaweza
kupata maelezo mbalimbali yatakayokuwezesha kujifunza mambo muhimu mbalimbali ikiwemo
utendaji wa kazi tofauti za ujenziBlog pia itakupatia ufahamu au elimu mbalimbali ya sheria za ununuzi,umiliki ardhi,viwango vya malipo na mambo muhimu ya kuzingatia kabla na wakati wa ujenzi n.k!
Blog pia inatoa nafasi kwa wadau wote na wasomaji,kutoa maoni yao,kutoa taarifa zozote muhimu zinazohisiana na ujenzi au makazi kama vile matatizo au kero zinazosababishwa na ujenzi holela.
Blog yetu pia inatoa nafasi kwa wadau watakaopenda kutangaza kazi au biashara zao.
Zaidi ya
yote,blog inakaribisha wamiliki wote
watakaopenda nyumba au majengo yao yaonyeshwe katika blog hii,kututumia
picha hizo,na maelezo watakayotaka yaambatane na picha hizo,kufanya hivyo
kupitia email yetu deco.tz@gmail.com au kuwasiliana nasi kwa maelekezo zaidi
kupitia namba +255 713 175 966.